# Ikawa Inatambulisha tukio jipya katika habari ya mzozo kati ya wafuasi wa Daudi na familia ya Sauli. # Nyumba ya Sauli Inaonesha familia ya Sauli na wafuasi waliochukuo umiliki wa maeneo yake alipokufa. # nyumba ya Daudi Inaonesha wafuasi wa Daudi. # Abneri akajipa nguvu katika nyumba ya Sauli Kuongezeka kwa nguvu ya Abneri juu ya familia ya Sauli kunasemwa kama alikuwa na nguvu za mwili. Yaani "Abneri akawa na nguvu zaidi juu ya familia na wafuasi wa Sauli" # Rizpa...Aiya Haya ni majina ya wanawake. # Ishboshethi Hili ni jina la kiume, mwana wa Sauli. # Kwa nini ulilala na suria wa baba yangu? Isboshethi anauliza swali hili kumkemea Abneri akifanya kama mfalme. Yaani "Haukuwa na haki ya kulala na suria wa baba yangu!" # kulala na Hili ni linalopunguza ukali wa neno likimaanisha kukutana kimwili.