# Maelezo kwa Ujumla Daudi anaimba wimbo wa maombolezo kwa Sauli na Yonathani # Wimbo wa Upinde Hili lilikuwa jina la wimbo # Kitabu cha Yashari Neno "Yashari" humaanisha "Unyofu." # iliyoandikwa katika Kitabu cha Yashari Hii ni taarifa ya mwanzo iliyoongezwa kumweleza msomaji yaliyotendeka katika wimbo # Utukufu wako, Israeli, umekufa "Utukufu wako" inamwonesha Sauli. # Wenye uwezo Kifungu "wenye uwezo" inamhusu Sauli na Yonathani. Kisifa nomino hiki kipo katika wingi, na kinaweza kutaarifiwa kama "wenye uwezo" # wameanguka Neno "wameanguka" linamaanisha "kufa" # Msisema katika Gathi...msiitangaze katika mitaa ya Ashkeloni Vifungu hivi viwili vinamaanisha jambo moja na vimerudiwa kama sehemu ya ushairi wa wimbo # Gath...Ashkeloni Gathi na Ashkeloni ni miwili kati ya miji mikubwa ya Wafilisiti. Wafilisiti walimwua Sauli na Yonathani # ili binti za Wafilisiti wasifurahi...ili binti za wasiotahiriwa wasisherehekehee. Vifungu hivi viwili vinamaanisha jambo moja na vimerudiwa kama sehemu ya ushairi wa wimbo. # binti za wasiotahiriwa kifungu hiki kinawahusu watu wasiomfuata Yahwe, kama vile Wafilisiti.