# Daudi akararua mavazi yake... watu waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile Daudi na watu wake walirarua mavazi yao kama ishara ya kuomboleza kwa ajili ya Mfalme Sauli. # alikuwa ameanguka Hii inamaanisha "alikuwa ameuawa." # Kwa upanga Hapa upanga unahusianishwa na vita, yaweza kumaanisha "katika magwanda ya kijeshi" # Unatoka wapi? Yule mtu alikuwa amekwisha eleza kuwa yeye ni Mwamaleki katika 1:8. Bila shaka Daudi anamwuliza yule mtu kuthibitisha kwa sababu ya hukumu kali aliyokuwa anaelekea kuitamka juu ya mtu yule.