# Akaniuliza, 'Wewe ni nani?' Nikamjibu, 'Mimi ni Mwamaleki.' Nukuu hii ingeweza kutaarifiwa kama kauli tendwa. Mfano "Aliniuliza mimi nilikuwa nani, nami nikamwambia kuwa nilikuwa Mwamaleki" # Mimi ni Mwamaleki Hawa ni watu walewale Daudi aliokuwa ametoka kuwashambulia katika 1:1. # shida kubwa imenipata Shida ya Sauli inasemwa kama kitu cha kutisha ambachokimemshikilia. Maana nyingine yaweza kuwa "nimeteswa vibaya sana" # uhai ungalimo ndani yangu Nahau hii inamaanisha kwamba yu ngali hai au "ningali hai" # asingeweza kuishi baada ya kuwa ameanguka "Hata hivyo angekufa tu"