# Hulda Hili ni jina la mwanamke. # Shalumu ... Tikva ... Harhasi Haya ni majina ya wanaume. # mtunza kabati la nguo Maana ziwezekanazo 1) mtu anayeangalia nguo ambazo makuhani huvaa katika hekalu au 2) mtu anayeangali nguo za mfalme. # aliishi Yerusalemu katika mtaa wa pili Hapa "theluthi ya pili" inarejea kwa sehemu mpya ambayo ilikuwa imejengwa kwa upande wa kaskazini mwa Yerusalemu. Pia, "aliishi Yerusalemu katika sehemu mpya ya Yerusalemu" # huyo mtu aliyekutuma kwangu Hapa "huyo mtu" inamrejea mfalme Yosia. # Nitaleta msiba mahali pake na kwa wenyeji wake Yahwe anafanya mambo mabaya yatokee imezungumzwa kana kwamba "msiba" ulikuwa kitu ambacho angekileta hiyo sehemu. # hapa mahali Hapa inarejea kwenye mji wa Yerusalemu ambao unawakilisha nchi yote ya Yuda.