# Maelezo ya Jumla: Sabau ya hukumu ya Yahwe juu ya Israeli kuendelea kuhusiana na historia nyuma yake. # Akawatoa "Akawatoa" ni picha ya kuwatoa kwa kikatili. "Yahwe aliwatoa watu wa Israeli" # kutoka kwenye ukoo wa kifalme wa Daudi "kutoka kwenye uzao wa Daudi" (UDB) # akawapeleka Israeli mbali na kumfuata Yahwe "aliwageuza watu wa Israeli mbali na kumfuata Yahwe" # hawakujiepusha nazo "Waisraeli hawakuacha kufanya hizi dhambi" au "Hawakugeuka kutoka kwenye hizo dhambo" (UDB) # basi Yahwe akawaondoa Israeli kutoka usoni mwake "Uso" ni picha ya umakini na kujali. "Basi Yahwe aliwaondoa watu wa Israeli kutoka kwenye uangalifu wake na utunzaji"