# Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda Inaweza kuelezwa wazi kwamba huu ni mwaka wa hamsini wa utawala wake. "Katika mwaka wa 50 wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda" # Pekahia Hili ni jina la kiume. # yaliyo maovu usoni mwa Yahwe Uso wa Yahwe unawakilisha hukumu ya Yahwe. # Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati Kuacha dhambi inawakilisha kuacha kuzifanya hizo dhambi. "Pekahia hakuacha kufanya dhambi za Yeroboamu mwana Nebati" au "kuasi kama Yeroboamu mwana wa nebati" # alisababisha israeli kuasi Hapa neno "Israeli" inawakilisha watu wa ufalme wa israeli.