# yalikuwa machungu sana Kuteseka ilikuwa vigumu ilizungumziwa kana kwamba ilikuwa ladha chungu. "ilikuwa chungu sana" # hapakuwa na mwokozi kwa ajili ya israeli "hapakuwa na mtu yeyote angeweza kuiokoa israeli" # kufuta Kuiangamiza Israeli kabisa inazungumziwa kana kwamba Yahwe amewasafisha kwa nguo. "angamiza kabisa" # jina la Israeli Hapa "jina la Israeli" linawakilisha Israeli yote na wenyeji wake. "watu wa Israeli" # chini ya mbingu "juu ya nchi" # aliwaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana Yehoashi Hapa "mkono" unarejea kwa uweza. Yeroboamu aliwashinda maadui wa Israeli kwa msaada wa jeshi lake. "alimuwezesha Mfalme Yeroboamu na jeshi lake kuwaokoa"