# Maelezo ya Jumla: Nabii mdogo anaendelea kunena maneno ya Yahwe kwa Yehu, ambaye alikuwa amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Israeli. # Nitaifanya nyumba ya Ahabu kama Hii inamaanisha kwamba Mungu atamwangamiza Ahabu na familia yake kama alivyomwangamiza Yeroboamu na Baasha na familia zao. "nitaiendesha nyumba ya Ahabu kama ninavyoiendesha ya" # nyumba ya Hili neno limetumika katika huu mstari mara tatu. Kila wakati, neno "nyumba" linarejea kwa "familia" ya mtu maalumu. "familia ya" # Nebati ... Ahiya Haya ni majina ya wanaume. # Mbwa watamla Yezebeli Hii inamaanisha kwamba mbwa wataila maiti yake. "Mbwa wataila maiti ya Yezebeli"