# kuyaponya haya maji Hii inamzungumzia Yahwe akifanya maji machafu kuwa masafi kana kwamba ameyaponya. "kufanya maji masafi" # hakutakuwa na kifo tena au nchi isiyozaa matunda Hii inarejea kwa vitu visababishwavyo kwa maji machafu. Hii inaweza kuandikwa pia katika mfumo chanya. "hakutakuwa na kifo tena au matatizo na mbegu zisababishwazo na haya maji" au "kutoka sasa juu ya haya maji yataleta uhai na kusaidia nchi kuzaa matunda" # maji yaliponya "maji yamebakia masafi" # hata leo ... aliongea Hii inamaanisha kwamba kitu kimebaki katika hali fulani hata wakati uliopo. "kwa neno ambalo Elisha aliongea, na kubakia siku zote masafi"