# Sentensi Unganishi Yohana anamalizia barua yake kwa kuonyesha shauku ya kuwatembelea na anatoa salamu kutoka kanisa jingine # Maelezo ya Jumla Maneno "kwako" yanaonyesha umoja katika mstari wa 12. Neno "yenu" linaonyesha wingi mstari wa 13 # sikutaka kuyaandika kwa karatasi na wino Yohana hakutaka kuyaandika mambo mengi lakini alitaka kuja kuongea nao ana kwa ana. # Watoto wa dada yenu mteule Yohana anazungumza habari ya kanisa jingine kana kwamba ni dada kwa kanisa analowaandikia na waumini wa kanisa hilo anawafananisha na watoto. Hapa inasisistiza kwamba waumini wote ni familia ya kiroho.