# Yeyote aendeleae mbele Hii inaonyesha mtu anaye dai kufahamu zaidi juu ya Mungu na ukweli kuliko mtu yeyote "Yeyote anayesema kuwa anafahamu zaidi kuhusu Mungu." au " Yeyote anayeikana kweli" # hana Mungu " si mali ya Mungu" # Yeye adumuye katika fundisho anaye Baba na Mwana "Wale wanaofuata mafundish ya Kristo ni mali ya Baba na Mwana" # Baba na Mwana Hivi ni vyeo muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu # msimkaribishe katika nyumba zenu Hapa ina maanisha kumkaribisha na kumtendea heshima ili kujenga uhusiano na naye. # hushiriki katika matendo yake maovu " Hushiriki naye katika matendo yake ya uovu" au" humsaidia katika matendo yake maovu."