# ...wewe, mwanamke, nakuandikia Ni maneno ambayo yametumiwa katika hali ya umoja. # kama vile tu tulivyoipokea amri hii kutoka kwa Baba "Kama vile Mungu Baba alivyo tuagiaza" # siyo kwamba nakuandikia amri mpya " siyo kwamba nakuagiza kufanya jambo jipya" # bali ile tuliyokuwa nayo tokea mwanzo Hapa neno "mwanzo" inamaanisha " tulipoamini kwa mara ya kwanza" kwa maneno mengine:- " lakini nawaandikia kama tulivyoagizwa na Kristo kufanya tulipoamini mara ya kwanza." # tunapaswa kupendana sisi kwa sisi. Hii inaweza kutafisiriwa kama sentensi mpya: "Na alitupa amri kwamba tunapaswa kupendana." # Hii ndiyo ile amri, kama mlivyoisikia tokea mwanzo, kwamba mnapaswa kuenenda katika hiyo. " Mungu amewaagiza tangu mwanzo mlipoamini mpendane"