# mapigo arobaini kasoro moja hii ilikuwa kawaida kueleza kuwa nimechapwa viboko 39. Viboko arobaini[40] inadhaniwa ni kuua mtu. # Nilipigwa kwa fimbo Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa kauli tendaji hivi: "watu walinipiga kwa viboko vya miti" # "nilipigwa kwa mawe" Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa jinsi hii:"watu walinitupia mawe mpaka wakadhania kuwa nimekufa" # Nimetumia usiku na mchana katika bahari wazi Paulo anazungumzia muda aliokuwa majini wakati meli ilipokuwa katika kuzama. # hatarini kwa ndugu za uongo "na hatari toka kwa wanaojifanya kuwa ndugu katika Kristo, lakini ni wametusaliti"