# Tunaona fahari juu ya hili..sababu yenu ya kujisifu "Maneno "kujisifu" na kuona fahari " yametumika hapa katika mtazamo chanya wa utoshelevu wa hisia kubwa na furaha katka kitu fulani. # ushuhuda wa dhamiri zetu Fikra za Paulo na Timotheo kuhusu matendo yao yashuhudia kwamba wameishi katika njia impendezayo Mungu. # siyo katika hekima ya kidunia Neno "ya kidunia" linaeleza kile kinachotambulisha jamii ya wanadamu ambayo haimchi Mungu. "siyo kwa kufuata hekima ya kibinadamu" # hatuwaandikii chochote msichoweza kukisoma au kukielewa Hii inaweza kuelezwa kuwa "Mnaweza kukisoma na kukielewa kila kitu tunachowaandikieni" # kama vile mtakavyokuwa wetu "Unaweza kuyagawa maneno "Sababu yetu kuona fahari" kujaza duaradufu. "kama mtakavyokuwa sababu yetu ya kuona fahari"