# Kama vile mateso ya Kristo yalivyoongezeka kwa faida yetu Paulo anazungumzia mateso ya Kristo kama vile yalivyokuwa kielelezo ambacho kingeongezeka katika idadi "Kama vile Kristo alivyoteswa sana kwa faida yetu" # Mateso ya Kristo Maana zake zaweza kuwa 1) kwamba hii ina maanisha mateso ya Paulo na Timotheo waliyoyapitia kwa sababu wanahubiri ujumbe unaomhusu Kristo au 2) inamaanisha mateso ya Kristo aliyoyapitia kwa niaba yao. # Faraja yetu inadumu Paulo anazungumza kuhusu faraja kwa vile kama mfano ambao ungeweza kuongezeka ukubwa wake. # lakini kama tukiteswa hapa neno "sisi" lina maanisha Paulo na Timotheo, lakini siyo Wakorintho. Hii inaweza kuelezwa katika kauli tendaji "Lakini hata kama watu wakitutesa" # Kama tukitiwa faraja Hii inaweza kuelezwa katika kauli tendaji badala yake " Kama Mungu akitufariji" # Faraja yenu inafanya kazi vizuri "Mnapitia faraja timilifu"