# Kauli Unganishi: Paulo anazungumza jinsi alivyotenda zamani na anamtia moyo Timotheo kumtumaini Mungu. # Nashukuru "Ninashukuru" au "mimi nashukuru kwa" # yeye aliniona mimi mwaminifu "yeye alinitazama mimi mwaminifu" au "alifikiria kuwa ninafaa" # na akaniweka katika huduma "na kuniweka katika nafasi ya kutumika" au "hivyo aliniteua katika huduma" # mimi, mtukana Mungu wa zamani "mimi, ambaye alisema maovu kinyume na Kristo" au "mimi, ambaye nilikuwa mtukana Mungu hapo zamani" # mtu wa vurugu "mtu ambaye anaumiza wengine." Huyu ni mtu anayeamini anayo haki kuumiza wengine. # Lakini nilipokea neema kwa sababu nilitenda kwa ujinga katika kutoamini NI: "Lakini kwa sababu sikuamini katika Yesu, na nilikuwa sijui nilichokuwa nikifanya, nilipokea neema kutoka kwa Yesu" # Nilipokea neema NI: "Yesu alinionesha neema" au "Yesu kashatoa neema kwangu" # Lakini neema "Na neema" # ilibubujika kwa imani na upendo "ilikuwa kwa wingi sana" au "ilikuwa zaidi kuliko ile ya kawaida"