# sasa Neno limetumika hapa kuonesha kituo kwenye mafundisho ya msingi. Hapa Paulo anaeleza lengo la kile anachomwamuru Tithotheo. # amri Hii haimaanishi Agano la Kale au Amri Kumi lakini zaidi ni wajibu uliotolewa na Paulo kwenye 1:3. # ni pendo Inawezekana kumaanisha 1) upendo kwa Mungu au 2) kuwapenda watu. # kutoka moyo safi Hapa "safi" inamaanisha kuwa mtu hana nia ovu ya kufanya mabaya. Na "moyo" hapa inamaanisha akili na mawazo ya mtu. # dhamiri nzuri "dhamiri ambayo imechagua haki juu ya mabaya" # imani thabiti "uaminifu" au "ukweli" au "isiyo na unafiki" # baadhi ya watu wamekosea Paulo anaongelea imani ndani ya Kristo kuwa shabaha yetu. # na wameasi vitu hivi "kuasi" kama ilivyotumika hapa ni msemo unaomaanisha kuwa watu wameacha kufanya maagizo ya Mungu. # walimu wa sheria Hii inamaanisha "sheria za Musa" # Lakini hawaelewi "ingawa hawaelewi" au "lakini hawaelewi"