# Maelezo ya jumla Paulo anaongelea waamini walio kufa, walio hai, na ao watakao ishi Kristo akirudi. # Hatutaki msielewe. "Tunataka muelewe" # Hatutaki "Sisi" inawaelezea Paulo, Silvanus na Timotheo lakini sio waamini wa Thesalonike. # Ndugu Hapa "ndugu" inamaanisha Mkristo mwenzako. # Kulala Hapa inamaanisha "kufa." # Msiomboleze "Msisikitike" # Kama hao wasiojua mambo yajayo "Kama watu wasioamini" # Kama tukiamini Hapa "sisi" linawaelezea Paulo na hadhira yake. # Kufufuka tena "kufufuka na kuishi tena" # Atawaleta pamoja na Yesu hao waliolala mauti. "akirudi atawafufua waamini waliokufa wakimwamini Yesu" # Kwa ajili ya hayo twasema "Sisi" linawaelezea Paulo, Silvanus na Timotheo lakini sio waamini wa Thesalonike. # Hakika hatutawatangulia "hakika hatutakwenda mbele yao"