# Taarifa ya jumla: Mwandishi anatupa taarifa kabla hajaendelea na simulizi. # Basi Daudi alikuwa amesema, "Hakika ... wa kwake" Msomaji anatakiwa aelewe kuwa Daudi alisema maneno haya kabla hajasema "Kila mtu afunge upanga wake" katika 25:12 # Basi Daudi Neno "basi" linaonesha kuwa mwandishi ameacha kuandika kuhusu Abigaili na akaanza kuandika kuhusu Daudi. # na vyote alivyonavyo hakuna kilichopotea "Bado anacho kila kitu ambacho ni chake" # Mungu na anitendee hivyo mimi "Mungu awapige adui wa Daudi" # wote wa kwake "watu wote ambao wako chini yake" au "wale wa familia yake"