# unao wakata manyoya "wakata manyoya wako wanafanya kazi" Daudi alitaka watu wake wamwambie hivi Nabali ili afahamu kuwa kondoo wake wapo salama kwa sababu watu wa Daudi waliwasaidia kuwalinda. # hatukuwafanyia ubaya, na hawakupotelewa kitu chochote Daudi anaonesha ni kwa namna gani yeye na watu wake waliwalinda watumishi wa Nabali na mifugo yao. # Basi vijana wangu wapate kibali machoni pako "Basi ukapendezwe na vijana wangu" # kwa mtumishi wako Daudi anaonesha heshima mbele ya Nabali kwa kuwaita watu wake watumishi wa Nabali. # mwanao Daudi Daudi anazungumza kama vile ni mtoto wa Nabali ili kuonesha heshima kwa Nabali aliyekuwa mtu mzima.