# Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake Daudi anajizungumzia mwenyewe kama "mtumishi wako" kuonesha heshima kwa Sauli. # alikuwa akichunga kondoo za baba yake "alikuwa akitunza kondoo wa baba yake" # dubu Dubu ni mnyama mkubwa mwenye miguu minne lakini anaweza kusimama na miguu miwili kama mtu. # Nilimfukuza na kumshambulia Hapa anazungumziwa simba au dubu. # na kumpokonya kutoka kinywani mwake Hapa anazungumziwa mwana kondoo. # aliponirukia "alinivamia" # nilimshika ndevu zake "ndevu" zinamuelezea simba au nywele zilizopo katika uso wa dubu.