# Agagi akafika kwake akiwa amefungwa minyororo "walimpeleka Agagi akiwa amefungwa minyororo" # Hakika uchungu wa kifo umepita "Kwa hakika sipo tena katika hatari au kufa" # Jinsi upanga wako ulivyofanya wanawake wapoteze watoto, vivyo hivyo mama yako naye hatakuwa na mtoto miongoni mwa wanawake Maneno haya yana maana moja "Kwa kuwa umewaua watu, wewe pia utauawa" # ulivyofanya wanawake wapoteze watoto, vivyo hivyo mama yako naye hatakuwa na mtoto "umewaua watoto wa wanawake wengine, hivyo nitamuua mtoto wa mama yako" # Kisha Samweli akamkata Agagi vipande vipande Samweli aliimaliza kazi ambayo Bwana alimuamuru Samweli alifanye.