# Mimi niko hapa , Nishuhudieni mbele za BWANA na mbele za mtiwa mafuta wake. Samweli anawasihi watu waeleze ikiwa amefanya jambo lolote baya. # Nimechukua ng'ombe wa nani? Nimechukua punda wa nani? Samweli anatumia maswali kuwakumbusha watu kuwa hakuwahi kuwaibia wanyama wao. # Ni nani nimemdhulumu? Samweli anatumia swali hili kuonesha kuwa amekuwa mkweli wakati wote. # Nishuhudieni, nami nitawarudishia "Ikiwa nimefanya mabaya yoyote semeni sasa na nitawalipa mnavyonidai."