# Bwana alikuja na kusimama Hii inaweza kuwa na maana ya 1) Bwana alimtokea Samweli na kusimama mbele yake au 2) Bwana alifanya uwepo wake uonekane kwa Samweli. # Mtumishi wako ana Samweli anazungumza na Bwana na kuonesha heshima. # ambalo masikio ya kila mmoja yakisikia yatashtuka Hapa "masikio ... yatashtuka" inamaanisha kuwa kila mtu atashituka kutokana na kitu atakachokisikia. # Kushtuka Kuhisi kama vile mtu anakuchoma na kitu chenye ncha au kushtuka kwa sababu mtu amepiga kibao sehemu fulani ya mwili.