# kila aliyezaliwa na Mungu "watoto wote wa Mungu" # huushinda ulimwengu "wanaushindi juu ya ulimwengu," "hufaulu dhidi ya ulimwengu," au "hukataa kufanya mambo maovu wayafanyayo wasioamini" # Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu: imani yetu "Imani yetu hupatia nguvu ya kuzuia lolote ambalo lingetutia katika ktenda dhambi dhidi ya Mungu" # Ni nani anayeushinda ulimwengu? Yohana alitumia swali hili kutambulisha jambo fulani alilotaka kufundisha. "Nitaambia anayeshinda ulimwengu" # ulimwengu ujumbe huu "ulimwengu? kwa kumaanisha watu wote wenye dhambi na mfumo mwovu wa ulimwengu" # Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Hili halimaanishi mtu maalum bali kwa yeyote anayeamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. # Mwana wa Mungu hiki ni cheo muhimu kwa Yesu kinachoelezea uhusiano wake kwa Mungu