# Malezo ya Jumla Hapa neno "yeye" "lake" humaanisha Mungu.(Tazama 1:5) # hatuna dhambi "hatutendi dhambi" # twajidanganya "Twajilaghai wenyewe" au "tunajiambia uongo wenyewe" # kweli haimo ndani yetu Ile kweli imezungumziwa kana kwamba lilikuwa ni jambo au kitu kambacho kingeweza kuwa ndani ya waamini. # kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote Virai hivi viwili kimsingi vinamaanisha jambo lile lile. Yohana anavitumia kusisitiza kwa hakika Mungu atasamehe dhambi dhambi. : "na atazisamehe kabisa kabisa ubaya ambao tumeufanya" # twamfanya yeye kuwa muongo, tunadai kwamba yeye ni mwongo: "ni sawasawa na kumwita yeye mwongo, kwa sababu amesema sisi sote tumetenda dhambi" # neno lake halimo ndani yetu Kutii kuheshimu neno la Mungu kumezunguziwa kana kwamba neno lake lilikuwa ndani ya waamini. : "hatulielewi neno la Mungu wala hatutii linachokisema"