# kuwa sitarajii kuwaona sasa Paulo anaeleza kwamba hataki kuwa na ziara ya ya muda mfupi, lakini anapenda kufanya ziara yamuda mrefu hapo baadaye. # Pentekoste Paulo alitarajia kubakia Efeso hadi sikukuu, iliyoanza mwezi Mei au Juni, siku hamsini baada ya pasaka. Baada ya hapo angesafiri kupitia Makedonia, na kufika Korintho kabla ya majira ya baridi yalioanza mwezi wa Novemba # mlango mpana umefunguliwa Hii inamaanisha kwamba Mungu amempa nafasi nzuri ya kuwafikia watu kwa injli.