# ameweka kila kitu chini ya miguu yake Wafalme walioshinda vita waliweza kuweka miguu yao juu ya shingo za adui zao waliowashinda. Kwa maneno mengine hapa inasema " Mungu amewaharibu kabisa maadui wote wa Kristo" # vitu vyote vimewekwa chini yake Maneno haya yakisemwa kwa kauli tendaji ni kwamba " Mungu amavitiisha vitu vyote chini ya Kristo" # mwana mwenyewe atawekwa chini Maneno haya yakisemwa kwa kauli tendaji ni kwamba " mwana mwenyewe atatiishwa" # mwana mwenyewe Katika mistari ya awali neno " mwana" linamaanisha " Kristo" : kwa maneno mengine ni kusema " Kristo ambaye ni Mwana wa Mungu" # Mwana...Baba Hivi ni vyeo muhimu vinavyofafanua uhusiano kati ya Yesu na Mungu.