# Sentensi Unganishi Baada ya kuzungumzia karama ambazo Mungu amewapa waumini, Paulo anasisitiza jambo la muhimu zaidi. # lugha...malaika Hapa inaweza kumaanisha 1) Paulo atumia lugha ya kukuza jambo ili ujumbe wake ueleweke, lakini hamaanishi kwamba wanadamu wanaweza kuongea lugha ambayo malaika hutumia. au 2) Paulo anafikiri kuwa baadhi ya watu ambao hunena kwa lugha huwa wananena lugha inayotumiwa na malaika. # nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao nimekuwa kama chombo kinachotoa sauti kubwa, sauti inayokera na kusumbua # upatu uvumao chombo chenye umbo la sinia, kinachofunikwa kwenye kitu kingine na kupigwa ili kutoa sauti. # ninautoa mwili wangu ili nichomwe moto kwa kutumia kitenzi tendaji ni sawa na kusema "ninawaruhusu watesi wangu wanichome moto hadi kufa"