# haimpasi mwanamume kufunika kichwa chake ikielezwa katika muundo tendaji, inaweza kumaanisha 1) "ni lazima mwanaume asifunike kichwa chake" au 2) " mwanaume hahitaji kufunika kichwa chake" # utukufu wa mwanaume Kama vile mwanaume anavyobeba taswira ya ukuu wa Mungu, mwanamke huonyesha tabia ya mwanaume. # Maana mwanamume hakutokana na mwanamke. Badala yake, mwanamke alitokana na mwanamume Mungu alimuumba mwanamke kwa mfupa kutoka kwa mwanaume. kwa maneno mengine " Mungu hakumuumba mwanaume kutoka kwa mwanamke . Badala yake Mungu alimuumba mwanamke kutoka kwa mwanaume"