# sentensi unganishi Paulo anawakumbusha waumini wa Korintho kwamba wanapaswa kuishi katika umoja na katika ujumbe wa msalaba wa Kristo, siyo ubatizo wa watu unaoleta wokovu. # kaka na dada zangu Hii inamaana washirika wote wakristo, ikijumuisha wote wanawake na wanaume. # kwamba wote mkubali " kuishi katika hali ya upatanifu na ushirikiano" # kwamba kusiwe na migawanyiko miongoni mwenu " kusiwe na migawanyiko ya makundi makundi miongoni mwenu" # kwamba muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi " muishi katika hali ya umoja" # watu wa nyumba ya Kloe Hii inahusu wanafamilia, wafanyakazi, na watu wengine ambao ni sehemu ya kaya ambayo Chloe ni mwanamke kiongozi. # kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu " kuna makundi yenye migogoro na kugombana kati yenu"