Malaika ni kiumbe wa kiroho aliyeumbwa na Mungu. Malaika wanaishi kwa kumtumikia Mungu kwa kufanya chochote anachowaambia kufanya. Jina "malaika mkuu" linamhusu malaika anayetawala au kuwaongoza malaika wote.
. Neno "Malaika mkuu" linamaanisha "mjumbe mkuu." Malaika pekee aliyetajwa kama "malaika mkuu" katika Biblia ni Mikaeli.
.Katika Biblia, malaika watoa ujumbe kutoka kwa Mungu. Jumbe hizi zinahusisha maelekezo jinsi Mungu alivyotaka watu wafanye.
>Pia malaika waliwaambia watu juu ya matukio yaliyokuwa yatendeke au yametendeka.
>Malaika wanamamlaka ya Mungu kama wawakilishi wake na wakati mwingine walizungumza katika Biblia kama vile Mungu mwenyewe alikuwa akiongea.
>Njia nyingine malaika wanatumika kwa kuwalinda na kuwatia nguvu watu
>Kirai maalumu, "malaika wa Yahwe" kina maana zaidi ya Moja: 1) Malaika anayemwakilisha "malaika anayemwakilisha Yahwe" au "mjumbe anayemtumikia Yahwe" 2)Yaweza kumhusu Mungu mwenyewe, anayeonekana kama mwanadamu alipoongea na mtu. Pengine moja kati ya maana hizi yaweza kuelezea matumizi ya "mimi" na malaika kama vile Mungu Mwenyewe alikua akiongea.
# bwana(lord), bwana(master), bwana(sir)
Neno "bwana" linamaanisha mtu mwenye umiliki au mamlaka juu ya watu.
>Neno hili wakati mwingine linatafasiriwa kama "bwana"(master) linapomweleza Yesu au linapomtaja mtu anayemiliki watumwa.
>Baadhi ya matoleo ya Kiingereza yanalitafasiri kama bwana(sir) katika mazingira ambapo mtu kwa heshima anamtaja mtu mwenye cheo cha juu.
# Jua, maarifa, kutambulisha
"Kujua" inamaanisha kufahamu kitu au kuwa na habari juu ya ukweli. "kujulisha" inamaanisha kusema habari.
>Neno "maarifa" lahusu habari anayoijua mtu. Yaweza kujua jambo katika ulimwengu wa roho au mwili.
"kujua kuhusu" Mungu yamaanisha kufahamu ukweli kumhusu yeye kwa sababu ya yaliyofunuliwa.
>"Kujua" Mungu inamaanisha kuwa na uhusiano naye. Hii pia inahusu kuwafahamu watu wengine.
>Kujua mapenzi ya Mungu yamanisha kufahamu alichokiagiza, au kufahamu anachotaka mtu afanye.
>"Kujua sheria" kujua alichokiagiza Mungu au kufahamu alichokielekeza Mungu katika sheria ya Musa.
>Wakati mwingine "maarifa" inatumika kama mbadala wa "hekima," inayohusisha kuishi katika hali inayompendeza Mungu.
"Maarifa ya Mungu" wakati mwingine inatumika kama mbadala wa "hofu ya Yahwe."