Ule msemo "mgeni" humrejelea mtu anayeishi katika taifa lisilo lake mwenyewe. Jina lingine la mgeni ni "mpitaji"
Katika Agano la Kale, musemo huu hasa humlenga yeyote anayetoka katika kikundi cha watu walio tofauti ya watu aliokuwa akiishi miongoni mwao.
Mgeni pia ni mtu ambaye lugha na utamaduni wake ni tofauti na ule wa kwako
Mathalani, Naomi na familia walipohamia Moabu, walikuwa wageni huko. Naomi na binti mkwe wake Ruthu walipohamia baadaye Israeli, Ruthu aliitwa :"mgeni" huko kwa sababu kwa asili hakutokea Israelli.
Kumpenda mtu mwingine ni kumjali mtu huyo na kufanya mambo yatakayomnufaisha yeye. Kuna maana mbali mbali za "upendo" ambazo baadhi ya lugha zinaweza kuuelza kwa kutumia maneno tofauti: 1. Upendo unaotoka kwa Mungu wenyewe hulenga juu mema kwa ajili ya wengine, hata kama haujinufashi wenyewe. Iana hii ya upendo hujali wengine, haijalishi wanafanya nini. Mungu mwenyewe ni pendo na ndiye asili ya upendo wa kweli.
3. Neno "upendo" pia laweza kumaanisha mapenzi baina ya mwanaumme na mwanamke. 4. Katika maelezo ya kitamathali , "Yakobo nimempenda, lakini Esau nimemchukia," ule msemo "nimempenda" humaanisha Mungu kumchagua Yakobo kuwa katika uhusiano naye wa kimaagano. Hili pia laweza kufasiriwa kama "aliyechaguliwa." Ingawaje Esau pia alibarikiwa na Mungu, hakupewa upendeleo wa kuwa katika agano. Ule msemo "nimemchukia" hapa umetumka kitamathali kumaanisha "aliyekataliwa" au "asiyechaguliwa."