sw_tn/psa/057/004.md

28 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maisha yangu yako katikati ya simba
Mwandishi anazungumzia adui zake kana kwamba ni simba. "Ninaishi katikati ya adui wakali" au "Adui wakali wananizunguka kama simba"
# wale walio tayari kunimeza
Kuangamiza inazungumziwa kama kumeza au kula kitu. Tafsiri zingine zinaelewa neno la Kihebrania kumaanisha "wanyam wa moto." Picha zote zinazungumzia adui zake kana kwamba ni wanyama pori. "wale walio tayari kuniangamiza"
# watu ambao meno yao ni mikuki na mishale
Mikuki na mishale ya wanyama inazungumziwa kana kwamba ni meno ya simba. Mwandishi wa zaburi anaendelea kuzungumzia adui zake kana kwamba ni simba. "watu wanaowaua wengine kwa mikuki na mishale kama simba wanavyoua kwa meno yao makali"
# mikuki na mishale
Hizi ni silaha za vita.
# ambao ndimi zao ni panga kali
Ulimi unawakilisha kile ambacho mtu anasemam na maneno mabaya ya adui yanazungumziwa kana kwamba ni panga. "ambao maneno yao ni kama panga kali" au "wanaosababisha taabu kubwa kwangu kwa sababu ya kile wanachosema"
# Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu
Mwandishi anamwomba Mungu kuonesha kuwa ameinuliwa. Kuinuliwa juu ya mbingu inawakilisha kuwa mkuu. "Mungu, onesha kuwa umeinuliwa juu ya mbingu" au "Mungu, onesha kuwa wewe ni mkuu katika mbingu"
# acha utukufu wako uwe juu ya dunia
Mwandishi wa zaburi anamwomba Mungu kuonesha utukufu wake. "onesha utukufu wako duniani kote"