sw_tn/psa/040/012.md

25 lines
786 B
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taabu zisizoweza kuhesabika zinanizunguka
Hapa taabu zinazungumziwa kana kwamba ni vitu vinavyomzunguka na kumtega mwandishi. "kuna taabu nyingi zimenizunguka kuliko navyoweza kuhesabu" au "taabu nyingi huja kwangu kuliko navyoweza kuhesabu"
# zisizoweza kuhesabika
Hii imeelezwa katika hali hasi kuweka mkazo wa idadi. "zilizo nyingi kwa idadi"
# udhalimu wangu
Hii inamaanisha matokeo ya dhambi. "matokeo ya udhalimu wangu"
# umenishika
Udhalimu wa mwandishi unazungumziwa kana kwamba ni adui zake wanaomdhuru.
# siwezi tena kuona kitu
Matoleo yanatofautiana katika kuelewa msemo huu. Inaweza kuwa inamaanisha kuwa mwandishi analia sana hadi hawezi kuona chochote kwa sababu ya machozi yake.
# moyo wangu umeshinda
Hapa "moyo" inamaanisha ujasiri wa ndani wa mwandishi.