sw_tn/isa/18/01.md

33 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Ole nchi yenye mchakarisho wa mabawa, ambayo ipo kando mwa mito ya Kushi
Maana za "mchakarisho wa mabawa" zawezekana kuwa 1) mabawa yanawakilisha mitumbwi ambayo ina matanga. "Ole wao ambao huishi katika nchi ng'ambo ya pili ya mito ya Kushi, ambao meli zao nyingi huonekana kama wadudu juu ya maji" au 2) mchakarisho wa mabawa una maana ya kelele ya wadudu wenye mabawa, huenda nzige.
# katika bahari
Mto ulikuwa mpana sana, na watu wa Misri na Kushi waliutaja kama "bahari". "katika mto mkuu" au "katika Mto"
# vyombo vya mafunjo
Mafunjo ni mmea mrefu ambao huota kando na Mto mkuu. Watu walifunga pamoja mafungu ya mafunjo kutengeneza makasia. "makasia ya mafunjo" au "makasia yanayotengenezwa kwa matete"
# taifa refu na laini ... watu wanaogopwa mbali na karibu ... taifa lenye nguvu na kukanyaga chini, ambayo nchi yake mito huigawanya
Misemo hii yote inaelezea watu wa taifa moja.
# taifa refu na laini
Neno "taifa" hapa lina maana ya watu wa taifa hilo. "taifa ambalo watu ni warefu na wana ngozi laini"
# watu wanaogopwa mbali na karibu
Maneno "mbali" na "karibu" yanatumika pamoja kumaanisha "kila mahali". "watu ambao wanaogopwa kila mahali" au "watu ambao kila mtu duniani huwaogopa"
# taifa lenye nguvu na kukanyaga chini
Kukanyaga chini inawakilisha kushinda mataifa mengine. "taifa ambalo lina nguvu na hushinda mataifa mengine"
# mito huigawanya
Huenda hii ina maana ya mito mingi ambayo hutiririka katika taifa ili igawanye katika sehemu tofauti.