sw_tn/isa/10/15.md

21 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Je! shoka litajivunia lenyewe dhidi ya yule anayelitumia? Je! msumeno utajisifu zaidi kuliko yule anayekata kwa kulitumia?
Msemaji anatumia maswali haya kukejeli mfalme wa Ashuru. "Shoka haliwezi kujivuna ya kwamba ni bora kuliko yule anayelishikilia. Na msumeno haupati utukufu zaidi ya yule anayekata kwa kulitumia"
# msumeno
kifaa chenye ncha kali kiinchotumiwa kukata mbao
# Ni kana kwamba kiboko kinaweza kuwainua wale ambao huiinua, au kana kwamba rungu ya mbao inaweza kumuinua mtu
Misemo hii ina maana moja na inatumika kuimarisha maana ya maswali mawili kabla yao. Inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Na wala fimbo au gongo haviwezi kumwinua yule anayeziokota"
# Kwa hiyo Bwana Yahwe wa majeshi atatuma udhoofishaji katika mahodari wake wa juu
Haipo wazi kama Yahwe au Isaya anazungumza. Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "kudhoofika" inaelezwa kama kitenzi "kufanya dhaifu". Kwa hiyo, Mimi, Bwana wa Yahwe wa majeshi, atafanya wanajeshi wenye nguvu wa mfalme kuwa dhaifu"
# chini ya utukufu wake kutachochewa mwako kama wa moto
Yahwe analinganisha adhabu yake kwa moto. Hii inasisitiza ya kwamba adhabu yake utaangamiza kabisa ufahari wote na ukubwa wa ufalme wa Ashuru. "Nitaangamiza ukubwa wake kana kwamba nilikuwa nikianzisha moto kuchoma kila kitu anachojivunia"