sw_tn/gen/08/20.md

65 lines
1.6 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# akajenga madhabahu kwa Yahwe
"akajenga madhabahu kwa makusudi ya Yahwe" au "akajenga madhabahu kwa ajili ya kumuabudu Yahwe." Inawezekana alijenga kwa mawe.
# wanyama walio safi ... ndege walio safi
Hapa "safi" ina maana ya kwamba Mungu aliruhusu wanyama hawa kutumika kama sadaka. Baadha ya wanyama hawakutumika kwa ajili ya sadaka na waliitwa "wasio safi".
# kutoa sadaka ya kuteketezwa
Nuhu aliwaua wanyama na kuwachoma kabisa kama sadaka kwa Mungu. "aliwachoma wanyama kama sadaka kwa Yahwe"
# harufu nzuri ya kuridhisha
Hii ina maana ya harufu nzuri ya nyama ya kuchomwa.
# akasema moyoni mwake
Hapa neno la "moyo" lina maana ya mawazo na hisia za Mungu.
# laani ardhi
"kuleta madhara makubwa kwenye nchi"
# kwa sababu ya mwanadamu
Hii inaweza kuwa wazi: "kwa sababu mwanadamu ni mwenye dhambi"
# nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto
"kutoka miaka yao ya utotoni wanakuwa wakifanya mambo maovu" au "walipokuwa wadogo, walitaka kufanya mambo maovu"
# nia za mioyo yao
Hapa neno "mioyo" lina maana ya mawazo, hisia, haja na ridhaa ya watu. "mwelekeo wao" au "tabia yao"
# tokea utoto
Hii ina maana ya mtoto mwenye umri mkubwa. "kutoka ujana wao"
# Wakati nchi isaliapo
"wakati nchi inapoendelea kudumu" au "Kadri nchi inavyoendelea kuwepo"
# majira ya kupanda mbegu
"msimu wa kupanda"
# baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi
Misemo hii miwili ina maana ya aina mbili za majira katika mwaka.
# kiangazi
kipindi kikavu na cha joto cha mwaka
# majira ya baridi
kipindi cha baridi kidogo na theluji katika mwaka
# havitakoma
"havitaacha kuwepo" au "havitaacha kutendeka" . Hii inaweza kuelezwa katika hali ya chanya. "vitaendelea"