sw_tn/2sa/07/10.md

37 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo ya Jumla
Yahwe anaendelea kueleza ahadi zake kwa Mfalme Daudi kupitia nabii Nathani.
# Nitateua mahali
"Nitachagua sehemu"
# nitawapanda pale
Yahwe anawafanya watu waishi katika nchi daima na kwa usalama inazungumzwa kama kama angewapanda katika nchi.
# na hawatasumbuliwa tena
Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji: Yaani: "na hakuna atakayewasumbua tena"
# kutoka siku
Hapa "siku" inawakilisha kipindi kirefu.
# Niliwaamru waamzi
Baada ya Waisraeli kuingia katika nchi ya Kanaani na kabla ya kuwa na wafalme wa kuwatawala, Mungu aliteua viongozi walioitwa "waamzi" kuwaongoza katika nyakati za shida.
# Nami nitakupa pumziko kutoka kwa adui zako wote...anakwambia kwamba atakutengenezea nyumba
Yaweza kufasiriwa: "Nami nitampa pumziko kutoka kwa adui zake wote... anamwambia kwamba atamtengenezea nyumba"
# Nikupumzisha kutoka kwa adui zako wote
"Nitakupa usalama kutoka kwa adui zako wote." Hapa "pumziko" ni nomino dhahania. Yaweza kuwa: "Nitawafanya adui zako wote waache kukushambulia"
# Nitakutengenezea nyumba
Maana hii hapa ya "nyumba" inarejea kwa wazao wa Daudi kuendelea kumiliki katika Israeli. Katika 7:3 Yahwe alimuuliza Daudi ikiwa angemjengea nyumba. Pale "nyumba" inawakilisha hekalu.