sw_tn/2sa/01/17.md

45 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo kwa Ujumla
Daudi anaimba wimbo wa maombolezo kwa Sauli na Yonathani
# Wimbo wa Upinde
Hili lilikuwa jina la wimbo
# Kitabu cha Yashari
Neno "Yashari" humaanisha "Unyofu."
# iliyoandikwa katika Kitabu cha Yashari
Hii ni taarifa ya mwanzo iliyoongezwa kumweleza msomaji yaliyotendeka katika wimbo
# Utukufu wako, Israeli, umekufa
"Utukufu wako" inamwonesha Sauli.
# Wenye uwezo
Kifungu "wenye uwezo" inamhusu Sauli na Yonathani. Kisifa nomino hiki kipo katika wingi, na kinaweza kutaarifiwa kama "wenye uwezo"
# wameanguka
Neno "wameanguka" linamaanisha "kufa"
# Msisema katika Gathi...msiitangaze katika mitaa ya Ashkeloni
Vifungu hivi viwili vinamaanisha jambo moja na vimerudiwa kama sehemu ya ushairi wa wimbo
# Gath...Ashkeloni
Gathi na Ashkeloni ni miwili kati ya miji mikubwa ya Wafilisiti. Wafilisiti walimwua Sauli na Yonathani
# ili binti za Wafilisiti wasifurahi...ili binti za wasiotahiriwa wasisherehekehee.
Vifungu hivi viwili vinamaanisha jambo moja na vimerudiwa kama sehemu ya ushairi wa wimbo.
# binti za wasiotahiriwa
kifungu hiki kinawahusu watu wasiomfuata Yahwe, kama vile Wafilisiti.