sw_tn/psa/144/009.md

32 lines
996 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# wimbo mpya
Maana zinazowezekana ni 1) "wimbo ambao hakuna mtu amewahi kuimba" au 2) "wimbo ambao sijawahi kuimba"
# kwako, unayewapa ...wafalme, uliyemwokoa
"kwako. Ni wewe unayewapa ... wafalme. Ni wewe ulimwokoa"
# Daudi mtumishi wako
Daudi anajizungumzia kana kwamba ni mtu mwingine. "mimi, Daudi, mtumishi wako"
# na upanga mwovu
Daudi anawazungumzia watu waovu kana kwamba ni upanga wanaotumia kama silaha. "kutoka kwa watu waovu waliokuwa wanajaribu kumuua"
# Niokoe na uniweke huru
"Tafadhali niokoe na uniweke huru"
# kutoka katika mkono wa wageni
Hapa "mkono" unaashiria nguvu."kutoka katika nguvu ya wageni"
# Midomo yao inazungumza uongo
"Wanazungumza uongo"
# mkono wao wa kuume ni uongo
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi anazungumzia utamaduni wa kuinua mkono wa kuume ili kuapa kuwa anachotaka kusema mtu mahakamani ni kweli, "wanadanganya hata wanapoapa kusema ukweli," au 2) "mkono wa kuume" ni sitiari ya nguvu, "kila kitu walichopata, wamepata kwa kusema uongo"