sw_tn/psa/092/010.md

16 lines
819 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Umeinua pembe langu kama pembe la nyati
Mwandishi wa zaburi anamzungumzia Mungu kana kwamba Mungu amemfanya kuwa na nguvu kama mnyama wa porini. "Umenifanya kuwa na nguvu kama nyati"
# Umeinua ... pembe
"Umenifanya kuwa na nguvu"
# Nimetiwa mafuta na mafuta mapya
Maana zinazowezekana ni kwamba mafuta ambayo Mungu ameweka juu ya mwandishi wa zaburi ni sitiari ya Mungu 1) kufanya kuwa mwenye furaha, "umenifanya kuwa na furaha sana" au 2) kumfanya kuwa na nguvu, "umenifanya kuwa na nguvu" au 3) kumwezesha kuwashinda adui zake, "umeniwezesha kuwashinda adui zangu."
# Macho yangu yameona anguko la adui zangu; masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu
Maneno "macho" na "masikio" ni njia nyingine ya kumaanisha mtu anayesikia na kuona. "Nimeona na kusikia kuhusu kushindwa kwa adui zangu waovu"