sw_tn/psa/091/003.md

20 lines
990 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Kwa kuwa atakuokoa kutoka katika mtego wa mwindaji na kutoka katika tauni hatari
"Kwa kuwa Mungu atakuokoa kutoka katika mtego wa mwindaji na atakuokoa kutoka katika tauni zinazoweza kuua"
# mtego wa mwindaji
"kutoka katika mtego ambao mwindaji aliweka kukushika"
# Atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio
Ulinzi wa Mungu hapa unazungumziwa kama "mbawa" ambazo ndege hutumia kufunika makinda yake dhidi ya hatari. "Atakufunika na mbwa zake" na "chini ya mbawa zake" zina maana moja. "Atakuweka salama na atakulinda"
# Uaminifu wake ni ngao na ulinzi
Uaminifu wa Mungu hapa unazungumziwa kama "ngao" ambayo inaweza kuwalinda watu wanaomtegemea. "Unaweza kumtumaini akulinde"
# ulinzi
Hakuna mtu anayejua kwa uhakika maana ya neno hili. Maana zinazowezekana ni 1) ngao ndogo iliyofungwa kwenye mkono wa askari inayotumika kujilinda dhidi ya mishale na panga au 2) ukuta wa mawe uliowekwa katika duara ambayo askari wanaweza kujificha na kupiga mishale.