sw_tn/psa/045/001.md

48 lines
1.7 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# weka katika Shoshannimu
Hii inaweza kuwa mtindo wa mlio wa muziki. wakati mwingine inatafsiriwa kama "weka katika mlio wa 'yungiyungi.'"
# Zaburi ya wana wa Kora
"Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika."
# Maschili
Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.
# Wimbo wa upendo
"Wimbo wa mapenzi"
# Moyo wangu umefurika kwa neno zuri
Mwandishi anazungumzia moyo wake kana kwamba ni chombo kinachofurika na kimiminiko. Neno "moyo" linawakilisha hisia zake, amabzo zinafurahishwa kwa nyimbo anazoimba. "Hisia zangu zinafuraha juu ya neno zuri"
# neno zuri
"wazo lenye uadilifu." Hii inamaanisha wimbo alioandika.
# niliyotunga
kuandika au kuunda wimbo
# ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi aliye tayari
Mwandishi anazungumzia ulimi wake kana kwamba ni kalamu. Anazungumza kwa ujuzi kama mwandishi mwenye uzoefu anavyoandika. "ulimi wangu ni kama kalamu ya mtu anayeandika vizuri" au "ninapozungumza kwa ujuzi kama mwandishi mwenye uzoefu anavyoweza kuandika maneno"
# Wewe ni mzuri kuliko watoto wa wanadamu
Msemo huu ni kukuza kwa neno na inasisitiza kuwa mfalme ni mzuri kwa mwonekano kuliko mtu mwingine. Msemo "watoto wa watu" ni lahaja inayomaanisha watu wote. "Una uzuri zaidi ya mtu mwingine yeyote"
# neema imemwagwa katika midomo yako
Mwandishi anazungumzia neema kana kwamba ni mafuta ambayo mtu ametumia kuitia mafuta midomo yake. Neno "midomo" linamaanisha maneno ya mfalme. Msemo huu unamaanisha kuwa mfalme anazungumza kwa ufasaha. "ni kana kwamba mtu ametia mafuta midomo yako kwa mafuta" au "unazungumza kwa ufasaha"