sw_tn/pro/01/07.md

32 lines
788 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo ya Jumla
baba anamfundisha mtoto wake.
# hofu ya Yahwe ni mwanzo wa maarifa
"Lazima umwogope Yahwe kwanza ili uanze kujua busara" au "lazima kumheshimu na kuwa na staha kwa Yahwe kwanza ili kujifunza busara"
# Yahwe
Hili ni jina lake Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale.
# wapumbavu hudharau hekima na mafundisho
"wale wasiothamini busara na maelekezo ni wapumbavu"
# wala usijiweke kando
Hii ni nahau kumaanisha " usipuuzie" au " usikatae"
# vitakuwa kilemba cha neema kwa ajili ya kichwa chako na mikufu yenye kuning'inia shingoni mwako
"yatakufanya uwe na busara kama kuvaa kilemba kwenye kichwa chako au mikufu kuzunguka shingo yako inavyokupendeza"
# kilemba
duara iliyofumwa kwa majani au maua
# mikufu
mapambo yanayovaliwa shingoni