sw_tn/job/38/19.md

24 lines
899 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo ya jumla
Yahweh aendelea kumtia changamoto Ayubu.
# sehemu ya kupumzikia kwa mwanga,
"sehemu ambayo mwanga hukaa" au " sehemu ambayo mwanga unaishi" Yahweh anauelezea mwanga kana kwamba alikuwa ni mtu.
# sehemu zake za kazi
"kwa mpaka wake' Mpaka huizunguka sehemu ya mwanga na giza. Wakati usiku unapoisha, giza hurudi katika sehemu yake. Na wakati siku inapoisha, mwanga hurudi katika sehemu yake.
# Bila shaka......kubwa sana!
Yahweh anatumia kejeli ya kinyume ili kutia mkazo kwamba Ayubu hauelewi mwanga na giza. "Ni wazi kwamba hauelewi kwa sababu ulikuwa bado haujazaliwa wakati nilipoviumba na haukuwa mtu mzima"
# kwa kuwa ulizaliwa wakati huo
Neno 'wakati" linarejelea muda ambao mwanga uliumbwa na kutengwa na giza. "kwa kuwa ulikuwa umezaliwa wakati nilipouumba ulimwengu"
# hesabu ya siku zako ni kubwa sana!
"umeishi miaka mingi sana ' au wewe ni mzee sana"