sw_tn/job/21/19.md

36 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Sentensi Unganishi
Ayubu anaendelea kuzungumza kwa rafiki zake.
# Ninyi mwasema
maneno haya yanaonesha kuwa Ayubu anawanukuu rafiki zake.
# Mungu huweka hatia ya mtu kwa ajili ya watoto wake kuilipa
Hatia inaongelewa kama kitu ambacho kinaweza kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Hapa kulipa inamaanisha adhabu kwa ajili ya dhambi. KTN: "Mungu hutunza kumbukumbu ya dhambi za mtu, kisha huwaadhibu watoto wa mtu huyo kwa matendo yake maovu"
# alipe yeye mwenyewe
Ayubu anaanza kutoa mawazo yake. KTN: " Lakini mimi nasema, alipe yeye mwenyewe"
# Macho yake mwenyewe yaone
"Macho" ni rejea kwa mtu.KTN: "aweze kuona yeye mwenyewe"
# anywe ghadhabu Mwenyezi
Ghadhabu ya Mungu inasema kana kwamba ni kinywaji ambacho mtu anaweza kuonja. Ayubu anataka waovu wapate adhabu ya Mungu.
# Kwani anajali nini kuhusu familia yake baada ya idadi ya miezi yake kuondolewa?
Ayubu anatumia swali kuonesha kuwa kuwaadhibu watoto wa mtu mwovu haina nguvu.KTN: "Kwani mtu mwovu hajali kuhusu familia yake baada ya kufa!"
# idadi ya miezi yake kuondolewa
hii ni namna ya staha kusema anapofariki.
# idadi ya miezi yake
Hii inarejea urefu wa miaka ya maisha yake.