sw_tn/jdg/09/19.md

32 lines
874 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Ikiwa mlifanya kwa uaminifu na uelekevu pamoja na Jerubalai na nyumba yake
Yotamu anaonesha kuwa kwa namna moja walichokifanya ni kitu kizuri japokuwa Yotamu haamini moja kwa moja kuwa wamefanya jambo zuri.
# Yerubaali
Hili ni jina lingine la Gideoni
# Nyumba yake
"nyumba" inawakilisha familia.
# Lakini ikiwa sio
Yotamu anaonesha upande mwingine kuwa wakichokifanya ni makosa na anatoa laana. Yotamu anaamini kuwa walichokifanya ni makosa.
# moto utoke kwa Abimeleki, ukawaangamize watu wa Shekemu
Yotamu anatoa laana. anazungumza juu ya Abimeleki kuwaharibu watu wa Shekemu kwa kuwaangamiza kwa moto.
# Basi moto utoke kwa watu wa Shekemu na Beth Milo, ili kumteketeza Abimeleki.
Yotamu anatoa laana. anazungumza juu ya Shekemu na Beth Milo kumteketeza Abimeleki kwa kumuangamiza kwa moto.
# Beth Milo
Hili ni jina la mahali.
# Beeri
Hili ni jina la mji