sw_tn/isa/51/19.md

36 lines
1.5 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo ya Jumla
Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.
# ni nani atasikitika pamoja na wewe? ... Nani atakufariji?
Isaya anatumia maswali kusisitza ya kuwa sasa hakuna mtu wa kulia pamoja nao au kuwafariji. Maswali haya yanweza kuandikwa kama kauli. "lakini hakuna mtu wa kulia pamoja nawe ... Hakuna mtu w kukufariji"
# Shida hizi mbili
Shida hizi mbili zina maana ya "ukiwa na uharibifu" na "njaa na upanga".
# ukiwa na uharibifu
Maneno haya yana maana moja na husisitiza uharibifu wa nchi unaosababishwa na jeshi pinzani. "adui zako wameacha miji tupu na kuharibiwa"
# njaa na upanga
Maneno "njaa" na "upanga" yanafafanua shida ambazo zitakuja juu ya watu. "Upanga" una maan ya "vita". "wengi wenu mmekufa kutokana na njaa na vita"
# wanalala katika kila kona ya mtaa
Huu n ujumla, ambayo ina maana ya watoto wengi watalala mitaani, lakini sio katika kila kona ya mtaa. "wanalala mtaani"
# kama paa ndani ya wavu
Hii inazungumzia watoto kuchoka sana na kutojiweza kana kwamba walikuwa paa waliokamatwa katika mtego. "hawajiwezi, kama paa aliyeshikwa katika wavu" au "kutojiweza kama paa aliyetegwa"
# paa
Huyu ni mnyama, anayefanana na mbawala, ambaye ana pembe na hukimbia haraka sana.
# wamejaa hasira ya Yahwe, karipio la Mungu wako
"hasira ya Yahwe" ina maana ya Yahwe kuadhibu watu wake kwa sababu ya hasira yake dhidi yao. Hii inazungumzia watu kuadhibiwa sana kana kwamba wamejaa hasira ya Yahwe. Pia, neno "karipia" linaweza kuandikwa kama kitenzi. "wameahibiwa sanana Yahwe kwa sababu alikuwa na hasira sana kwao na kuwakaripia"